UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hauna papara na mchezaji wa kikosi hicho Gadiel Michael ambaye amegoma kusaini ndani ya klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla amesema kuwa kwa sasa Yanga imefanya usajili wa maana hivyo hawawezi kusumbuliwa na mchezaji mmoja.
“Tumefanya usajili makini msimu huu, kama mabeki tunao mtu kama All Sonso na Ally Ally hawa wote wapo vizuri kucheza nafasi yake, ila mpango wetu ni kuwa na wachezaji wawili kila upande.
“Kama ataamua kuondoka milango ipo wazi hatuna kazi ya kumbebeleza mchezaji kwani dirisha dogo ni karibu tutasajili wachezaji wengine,” amesema.