Uncategorized

NAHODHA WA TIMU YA TAIFA AJIVUNIA UWEZO WA WACHEZAJI WENZAKE

admin July 5, 2019 1:51 pm
NAHODHA wa timu ya Tanzania, Mbwana Samatta amesema kuwa licha ya kupoteza michezo yote waliyocheza kwenye michuano ya Afcon bado anajivunia uwezo wa wachezaji wenzake.

Stars imetolewa kwenye michuano ya Afcon baada ya kucheza michezo yote mitatu bila kujikusanyia pointi huku ikikubali kufungwa jumla ya mabao nane na kufunga mabao mawili pekee.

“Haikuwa lengo letu kufanya vibaya, tulipambana kwa kadri ya uwezo wetu mwisho wa siku tukashindwa, ila ninajivunia uwezo wa wachezaji wenzangu wamefanya kitu kikubwa nina amini wakati ujao tutafanya vizuri,” amesema Samatta.

Stars ilikuwa kundi C pamoja na Kenya, Senegal na Algeria na mbili zilizofuzu hatua ya 16 bora ni Senegal na Algeria.
PAUL POGBA AIKAZIA MANCHESTER UNITED, KUOMBA ASEPE ZAKE MSIMU UJAO YANGA WAMTAJA MBADALA WA GADIEL MICHAEL

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply