Uncategorized

NYOTA WA SIMBA KUTIMKIA SINGIDA UNITED

admin July 8, 2019 9:07 am

NYOTA wa Simba, Marcel Kaheza ambaye mkataba wake na AFC Leopards ya Kenya alikokuwa kwa mkopo umemalizika kwa sasa ameingia rada za Singida United ambao wanasuka kikosi upya.

Hesabu za Singida United zilikuwa kuipata saini ya mshambuliaji Rashid Juma kutokana na ugumu wa kumpata nyota huyo wameshusha majeshi yao kwa Kaheza.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa mpango wa usajili kwa sasa ndani ya Singida United umepamba moto hivyo kama jina la nyota huyo limo kwenye ripoti ya mwalimu watamnasa.

“Tunasajili kwa mapendekezo ya mwalimu hivyo kama atatuambia tumsajili Kaheza tutazungumza naye kwani hakuna kinachoshindikana kikubwa ni kuwa na timu bora itakayoleta ushindani,” amesema.

EXCLUSIVE: PAMOJA NA MATUSI YA AMUNIKE, SAMATTA ALIOKOA JAHAZI YONDANI KURUDI UWANJANI, UGOMVI WAKE NA BANDA HUU HAPA-2 LIGI KUU BARA KUANZA KUTIMUA VUMBI AGOSTI, ISHU YA VIPORO YAPATA DAWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply