Uncategorized

GADIEL MICHAEL APANIA KUFANYA MAKUBWA NDANI YA SIMBA

admin July 11, 2019 6:43 am

GADIEL Michael nyota mpya wa Simba amesema kuwa kazi yake kubwa ni kucheza hivyo atapambana kufanya vizuri ndani ya kikosi chake kipya.

Michael amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea Yanga hivyo msimu ujao atakuwa ndani ya kikosi cha mabingwa hao kutetea ubingwa wa Simba.

“Kazi yangu kubwa ni kucheza na siwezi kuchagua kazi, nipo tayari kupambana na changamoto mpya hivyo ni wakati wangu kuonyesha uwezo wangu zaidi,” amesema.

Michael anaungana na nyota wenzake wawili ambao wametoka Yanga na kufanya jumla wawe watatu ambao ni Ibrahim Ajib na Beno Kakolanya.

GAZETI LA SPOTI XTRA KATIKA UKURASA WA MBELE LEO ALHAMIS, BIGIRIMANA AANZA NA AJIBU SIMBA YAMPELEKA MO KWA WAZIRI MKUU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply