Uncategorized

SIMBA YAMPELEKA MO KWA WAZIRI MKUU

admin July 11, 2019 7:58 am


KIUNGO wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Mo’ ametolewa kwa mkopo rasmi na klabu yake kwenda kujiunga na Namungo FC ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu. Mo amejiunga na klabu ya Namungo FC ambayo mlezi wake ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na imepanda ligi kuu.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa anahusishwa kwenda kwa mkopo KMC, ni moja kati ya wachezaji wa simba ambao msimu uliopita walishindwa kutamba ndani ya kikosi hicho.

Meneja wa  nyota huyo, Jamal Kisongo alisema; “Msimu ujao Mo hatakuwa sehemu ya kikosi cha simba atakuwa  katika kikosi cha Namungo FC ambako ametua kwa mkopo na atacheza hapo kwa msimu huo mpya.

“Yalikuwa makubaliano yetu na simba ndiyo maana hata kwenye majina ambayo wamepeleka Caf  hakuna jina lake anaenda timu nzuri kikubwa ni yeye kupambana.”

GADIEL MICHAEL APANIA KUFANYA MAKUBWA NDANI YA SIMBA WABABE SENEGAL NA NIGERIA WATINGA NUSU FAINALI AFCON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply