Uncategorized

YANGA, SIMBA KUKAMULIWA ‘MIDOLA’ NA TFF

admin July 12, 2019 11:20 am


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezitaka timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kukamilisha usajili Kwa njia ya mtandao (Tanfootball Connect) kabla ya usajili kufungwa kwani timu nyingi zimekuwa zikisuasua kukamilisha usajili wao kwa wakati. 

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo amesema kuwa mpaka sasa hakuna timu ambayo imekamilisha kiukamilifu zoezi la usajili kwa mtandao.

“Timu nyingi zinazoshoriki Ligi Kuu Bara hazijakamilisha usajili Kwa njia ya mtandao hivyo dirisha likifungwa hakutakuwa na muda wa nyongeza, kila timu itakayochelewa kukamilisha usajili faini itahusika.

“Usajili wa kwa timu zinazoshoriki mashindano ya Caf bila faini umefungwa Julai 10 hivyo kuanzia Julai 11 mpaka 21 watatoa faini ya dola 250 watakaoendela mpaka Julai 30 watatoa faini dola 500 na wachezaji hao watacheza mzunguko wa pili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Ndimbo.
SIMBA YAMPELEKA MCHEZAJI YANGA HOSPITALI SIMBA YAKUBALI KUPIGWA FAINI YA USAJILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply