Uncategorized

KAGAME YAWAPA SOMO KUBWA KMC KIMATAIFA

admin July 14, 2019 10:58 am


UONGOZI wa KMC umesema kuwa ushiriki wao michuano ya Kagame umewapa fursa ya kujifunza mambo mengi hasa kuelekea kwenye michuano ya kimataifa ambayo itashiriki.

KMC ilialikwa kwenye michuano ya Kagame inayoendelea nchini Rwanda imetolewa hatua za awali baada ya kukusanya pointi nne.

Kwenye kundi A KMC ilishinda mchezo mmoja dhidi ya Rayon Sport na ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Atlabara na ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe.

Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa hawajatoka mikono mitupu licha ya kushindwa kutinga hatua ya robo fainali.

“Tumejifunza mengi na mashindano haya yametupa picha halisi ya huko tuendako, ushindani ulikuwa mkubwa mpaka hapa tulipofika si sehemu mbaya, tumepata uzoefu utakaotusaidia kwenye michuano ya kombe la Shirikisho pamoja na Ligi Kuu Bara,” amesema.

AJIBU AWATETEMESHA KAHATA NA CHAMA SIMBA KESI YA MALINZI NGOMA BADO MBICHI, UAMUZI WA KESI SASA JULAI 23

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply