Uncategorized

SIMBA HAWAPOI, WABAINISHA MALENGO YA TIMU MSIMU UJAO

admin July 14, 2019 11:33 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa malengo makubwa kwa msimu ujao ni kuleta ushindani mkubwa utakaoifanya klabu kuwa ndani ya timu tano kubwa barani Afrika.

Simba leo wana semina ya ndani ya wachezaji wa Simba pamoja na benchi la ufundi inayofanyika ilipo kambi yao iliyopo kwenye fukwe za Bahari ya Hindi ambayo inahusu historia ya klabu, kanuni, maadili, desturi, malengo ya mwaka 2019-20 na nidhamu.

Mulami Nghambi ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba amesema kuwa “Tunataka kuwa moja ya timu tano bora Afrika na ili kufika huko kuna mambo mengi yanahitajika kufanyika,” amesema.

Beki wa Simba, Gadiel Michael ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea Yanga amesema kuwa kazi kubwa kwa wachezaji ni kushirikiana kutafuta mafanikio.

KESI YA MALINZI NGOMA BADO MBICHI, UAMUZI WA KESI SASA JULAI 23 WACHEZAJI YANGA WAPIGWA STOP

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply