Uncategorized

AZAM FC: KESHO HAO MANYEMA WANAKAA

admin July 18, 2019 5:46 pm


IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kesho watapambana kuwakalisha wapinzani wao Manyema FC kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Kagame.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa wametambua ubora na uimara wa wapinzani wao hivyo watawamaliza mapema.

“Wapinzani wetu wapo imara, tumewaona kwenye mchezo wao dhidi ya APR, sasa tumejipanga kupata matokeo chanya hasa ukizingatia ni hatua ya nusu fainali hivyo kikubwa ni sapoti na kujituma,” amesema Cheche.

Azam FC ni mabingwa watetezi wa kombe la Kagame wametinga hatua ya nusu fainali baada ya kuwanyoosha TP Mazembe mabao 2-1.
VYAMA VYA MIKOA, TFF TUWEKEENI MAZINGIRA RAFIKI KWA MCHEZO WA SOKA NYOTA WANNE WA SIMBA WATUA AFRIKA KUSINI, WAANZA KAZI RASMI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply