Home Uncategorized MABINGWA WA AFRIKA ALGERIA WANATISHA KINOMA

MABINGWA WA AFRIKA ALGERIA WANATISHA KINOMA


ALGERIA mabingwa wapya wa Afrika wanatisha kwani licha ya wapinzani wao Senegal kutawala mchezo kwa kupiga jumla ya pasi 320 huku wao wakipiga jumla ya pasi 201 bado walilinda bao lao.

Bao la mabingwa hao lilifungwa kwa shuti kali lililopigwa na Bagdad Bounebdjah na lilimgonga beki wa Senegal, Cheikhou Kouyate kabla ya kuzama nyavuni.

Jitihada za mshambuliaji Sadio Mane hazikuzaa matunda kwani licha ya kupambana na kuiongoza safu yake ya ushambuliaji kupiga jumla ya mashuti 11 langoni huku mabingwa hao wakipiga shuti moja hakuna kilichobadilika.

Algeria wanaingia kwenye orodha ya timu zilizotwaa ubingwa huo mara mbili huku Senegal wakiingia kwenye rekodi ya timu zilizoingia kwenye fainali ya michuano hiyo mikubwa mara mbili.

SOMA NA HII  NYOTA MPYA YANGA NTIBANZOKIZA ATOA KAULI YA MATUMAINI