Uncategorized

HICHI NDICHO KILICHOWAFELISHA SENEGAL AFCON 2019

admin July 21, 2019 11:02 am

NYOTA wa timu ya Taifa ya Senegal, Sadio Mane amesema kuwa kilichowaponza washindwe kutwaa kombe la Afcon mwaka 2019 ni kushindwa kutumia nafasi walizozipata.

Senegal imetinga hatua ya fainali ya michuano ya Afrika mara mbili na imeambulia patupu muda wote.

Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2002 na ilifungwa na Cameroon kwa penalti nchini Mali na fainali yake ya pili ikafungwa na Algeria bao la mapema kabisa dakika ya pili nchini Misri.

Mane amesema kuwa kilichowaponza washindwe kupata ushindi ni kushindwa kutumia nafasi walizozipata jambo lililowafelisha.

“Tumeshindwa kutwaa kombe kutokana na kushindwa kutumia nafasi tulizozipata, wenzetu mapema walitumia nafasi waliyoipata hapo ndipo tulipokwama na inaumiza kweli,” amesema.

Algeria mara ya mwisho kutwaa taji hilo ilikuwa ni  mwaka 1990 na wamelitwaa tena mwaka 2019 baada ya kupita miaka 29.

REAL MADRID YATAKA BALE ASEPE, ZINEDINE APEWA JUKUMU HILO YANGA YATAJA KINACHOMKWAMISHA KIPA MPYA WA KENYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply