Uncategorized

AZAM FC WAO KIMATAIFA RATIBA YAO IMEKAZA NAMNA HII

admin July 22, 2019 8:22 am


KUMEKUCHA kimatafa ambapo mabingwa wa kombe la Shirikisho Azam FC, itaenyana na Fasil Kenema ya Ethiopia kwenye raundi ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo wa kwanza itakuwa ugenini kwenye mji wa Gondar, Ethiopia kati ya Agosti 9-11, huku ikimaliza kazi katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kati ya Agosti 23-25 mwaka huu.

Kama Azam FC itapenya kwenye raundi ya kwanza watakutana na mshindi wa jumla wa mechi kati ya Triangle FC ya Zimbabwe na Rukinzo ya Burundi, ikianzia nyumbani kati ya Septemba 13-15 kabla ya kurudiana ugenini Septemba 27-29, mwaka huu.

Ikitokea wakatusua kiunzi hicho basi watakuwa wamebakisha raundi ya mwisho ya mtoano kabla ya kuingia hatua ya makundi, na hapo itatarajia kucheza na moja ya timu zilizotolewa kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

HUYU NDIYE MBADALA WA LEROY SANE NDANI YA BAYERN MUNICH KMC KIMATAIFA USO KWA USO NA NYOTA WA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply