Ligi Kuu Zanzibar 2026
Michezo Bongo

SABABU ZALTAJWA: ZBL Yongeza Viwanja 3 Vipya Ligi Kuu Zanzibar 2026

Vardo August 26, 2026 5:35 pm

BODI ya Ligi Zanzibar (ZBL) imeweka wazi sababu za kuongeza viwanja vitatu vipya vitakavyotumika kwenye mechi za Ligi Kuu Zanzibar kwa msimu wa 2026-2027, lengo kuu likiwa ni kufikisha soka kwa mashabiki wa vijijini na kuwahi maandalizi ya AFCON 2027.

Viwanja hivyo vipya vilivyoongezwa ni pamoja na:

  • Kinyikani (Pemba)

  • Pangatupu (Unguja)

  • Kitogani (Unguja)

Ongezeko hili linafanya Ligi Kuu Zanzibar sasa kuchezwa kwenye jumla ya viwanja sita (6), ikilinganishwa na viwanja vitatu vilivyotumika awali ambavyo ni Gombani (Pemba), Mao A na Mao B (Unguja).

Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Zanzibar, Issa Kassim Ali, alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubaini kuwa mashabiki wengi wa mpira wa miguu wanakaa nje ya mji na walikuwa wakikosa fursa ya kushuhudia mechi hizo mubashara.

“Ligi ya Zanzibar itachezwa katika viwanja sita msimu huu ambavyo ni Gombani, Kinyikani, Pangatupu, Kitogani, Mao A na Mao B. Tunahitaji kuwafikia wapenzi wa mpira waliopo vijijini,” alisema Issa Kassim.

Kujiandaa na AFCON 2027

Mbali na kuwafikia mashabiki wa vijijini, Mtendaji Mkuu huyo alibainisha kuwa uboreshaji wa miundombinu unaofanywa na Serikali unasaidia kupanua wigo wa ligi hiyo na kukuza vipaji vya vijana maeneo mbalimbali.

Pia, uwepo wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) ambazo Tanzania itaziratibu kwa kushirikiana na Kenya na Uganda, ni sababu nyingine iliyosukuma ZBL kuongeza viwanja ili kumaliza ligi mapema na kupisha maandalizi ya mwisho ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

AFCON 2027: Zanzibar Yajipanga Kivingine, Miundombinu Na Fursa Za Kiuchumi Kuruha Mafunzo FC Yashusha Wachezaji 8 Wapya Ligi Kuu Zanzibar 2026/2027