Uncategorized

DAVID DE GEA ANUKIA KUWA NAHODHA WA UNITED

admin July 23, 2019 6:02 am


David De Gea anaweza kuwa nahodha wa Manchester United kutokana na moja ya kipengele kilichopo kwenye mkataba wake mpya anaotaka kusaini wa miaka sita ambao utamfanya awe kipa ghali namba moja duniani.

Ole Gunnar Solskjaer meneja wa Manchezter United yupo tayari kumkabidhi kitambaa cha unahodha kipa huyo baada ya nahodha wa awali Antonio Valencia kuondoka klabuni msimu uliopita.


“Nilimpa unahodha kwa baadhi ya mechi, ni sahihi na anavutia kuwa kiongozi kwa klabu kama Manchester United na anaweza kuilinda hii nembo. Kwahiyo anaweza kuwa nahodha, na nitafurahi akiwa nahodha,” amesema.

De gea amekuwa imara langoni tangu ajiunge na timu hiyo mwaka 2013 chini ya Alex Fergueson na kushinda kombe la ligi kuu kwa mara ya mwisho mwaka huo amedumu kwa misimu nane.

YANGA: MSIMU UJAO MAMBO NI MOTO KMC: TUPO TAYARI KUPAMBANA KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply