UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa tayari umeanza maandalizi ya kujiaanda na michuano ya kimataifa kweye kombe la Shirikisho.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azm FC, Jaffary Maganga amesema kuwa Kocha Mkuu ameaacha programu maalumu ambayo itatumika na wachezaji.
“Kocha Mkuu ameacha programu maalumu ambayo inaendelea na lengo ni kujiweka tayari kwa ushindani.
“Tutacheza na Fasil Kenema ya Ethiopia mchezo wetu wa kwanza kati ya Agosti 9/11 na marudiano itakuwa kati ya Agosti 23/25, tupo tayari,” amesema.
Ettiene Ndayiragije ambaye ni Kocha Mkuu wa Azam amepewa majukumu ya kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania inayojiaanda kushiriki michuano ya Chan Julai 28 dhidi ya Kenya.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.