Home Uncategorized SASA YANGA KUKIPIGA NA WALE WALIOITOA SHOO EVERTON YA ENGLAND

SASA YANGA KUKIPIGA NA WALE WALIOITOA SHOO EVERTON YA ENGLAND




Ikiwa ni katika kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi, Yanga imepanga kucheza mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wababe wa Everton FC ambao no Kariobang Shark’s ya nchini Kenya.


Wiki hiyo ya Mwananchi iliyopewa jina la ‘ Kukusanya Kijiji’ kilele chake kinatajiwa kuhitimishwa Agosti 4, Mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Kariobang hivi karibuni walicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Everton na kutoka sare ya bao 1-1 mchezo uliopigwa Kenya kabla ya kupigiana penalti na Kariobang kushinda mabao 4-3.


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela alisema kuwa wanacheza na Kariobang baada ya AS Vita ya DR Congo kuomba hudhuru ya kuingiliwa na ratiba ya Caf.


Mwakalebela alisema Mara baada ya kupokea barua hiyo ya hudhuru haraka wakazungumza na Kariobang na kukubali kuja nchini kucheza mchezo huo utakaopigwa saa kumi kamili jioni.


“Maandalizi ya Wiki ya Mwananchi inakwenda vizuri na siku hiyo tunatarajia kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Kariobang ambao walitufunga kwenye michuano ya SportPesa Super Cup.


” Hivyo mchezo huo kwetu tunauchukulia wa umuhimu kwa ajili ya kulipa kisasi,”alisema Mwakalebela.

Kwa upande wa katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki hiyo ya Mwananchi, Deo Mutta alisema kuwa “Uzinduzi ya Wiki ya Mwananchi itaanza rasmi Julai 27, mwaka huu kwa baadhi ya wanachama wa Yanga kwenda Zanzibar kutembelea kaburi ya muhasisi wa Yanga, Abeid Amani Karume na baada ya hapo jioni tutacheza mchezo wa kirafiki wa wanachama.


“Siku inayofuata tutarejea Dar na kuanza kukusanya kijiji kwa kuanza kutembea na gari kubwa la wazi lq GSM litakalokuwa na wasanii wa bongo fleva na movies.


“Gari hilo la wazi litaanzia safari zake Klabuni na kwenda Morocco, Mwenge, Bunju, Bagamoyo, Kiwangwa, Msata, Lugoba, Msoga na Mdaula na baadaye kwenda Morogoro na kurejea tena kwa kupitia njia ya Kimara na.Mbezi,” alisema Mutta.
SOMA NA HII  SIMBA YAKOMAA NA MZAMBIA, HILO DAU NI PASUA KICHWA