Uncategorized

KOCHA YANGA AMTAJA MLINDA MLANGO ATAKAYEANZA LANGONI

admin July 27, 2019 8:35 am

KOCHA wa makipa ndani ya Yanga, Peter Manyika amesema kuwa magolikipa wake wote wapo vizuri kwa ajili ya msimu ujao.

Manyika kwa sasa ana makipa watatu ambao ni pamoja na Farouk Shikalo, Ramadhan Kabwili na Klaus Kindoki ambao wote wanapambania kuwa namba moja.

Manyika amesema kuwa :”Kila mmoja anapambana kwa uwezo wake na kwa programu ambayo nimewapa nina imani wote watakuwa vema msimu ujao.

“Nimewaambia kwamba yule atakayefanya vizuri ndiye mwenye nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza msimu ujao,”.

Kwa sasa Yanga ipo kambini Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 23.

KOCHA STARS: MAJEMBE YA KAZI YAPO SAWA, AWAPA TANO NYOTA WA SIMBA KIPA STARS ATAMBA KUWAZUIA WASHAMBULIAJI WA KENYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply