Uncategorized

YANGA YATAKA MAJEMBE HAYA MAWILI, MMOJA KUMCHOMOA KUTOKA SIMBA

admin July 27, 2019 10:31 pm


UONGOZI WA Yanga umesema kuwa bado upo sokoni kusaka majembe mengine makali kwa ajili ya msimu ujao.

Dirisha la usajili linafungwa Julai 31 na Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kupitia kwa Ofisa Habari Clifford Ndimbo amesema kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa kuna nafasi mbili kwa sasa zimebaki kwa ajili ya kusajili.

“Bado usajili haujafungwa ni mpaka Julai 31 ndipo usajili unafungwa, nasi pia tumebakiza nafasi mbili kwa ajili ya usajili,” amesema.

Inaelezwa kuwa wachezaji ambao wapo kwenye hesabu kwa sasa ni pamoja na Bakari Mwanyento wa Coastal Union ambaye ni beki pamoja na Asante Kwasi.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI NAHODHA STARS: TUNAPENYA LEO MBELE YA KENYA, MASHABIKI MTUPE SAPOTI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply