Uncategorized

KMC YAONYOOSHA MABAO 2-1 KARIOBANG SHARK

admin August 6, 2019 7:51 am


KIKOSI cha KMC leo kimeibuka kidedea kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Kariobang Sharks uliochezwa uwanja wa Uhuru.

Ofisa Habari wa KMC, Anwar Bide amesema kuwa ni mwanzo mzuri  kwao kuelekea mchezo wa kimataifa dhidi ya AS Kigali utakaochezwa Agosti 10.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani ila mwisho wa siku tumeibuka na ushindi wa mabao 2-1 ni mwanzo mzuri kwetu kwa ajili ya michezo yetu ya kimataifa na tuna imani ya kufanya vizuri,” amesema.

Mabao ya KMC yamepachikwa kimiani na Serge Nogues pamoja na Vitalis Mayanga.

SIMBA: TUTAKACHOFANYA SISI WAPINZANI WETU YANGA HAWAJAKIFANYA NA NI NOMA LEO WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MGENI RASMI LEO UWANJA WA TAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply