Uncategorized

BEKI TANZANITE AWEKA REKODI TAMU, KILA MECHI ANACHEKA NA NYAVU, ANA TUZO MOJA YA MCHEZAJI BORA

admin August 9, 2019 4:39 am


ENEKIA Kasonga,beki kisiki wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ ameweka rekodi tamu kwenye michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini.

Tanzania imealikwa kwenye michuano hiyo na imetinga hatua ya fainali na itamenyana na Zambia mchezo wa fainali kumtafuta bingwa.

Kasonga amecheka na nyavu mara nne katika mechi nne ambazo Tanzanite imecheza mpaka sasa ambapo ni katika mchezo dhidi ya Botswana ambapo Tanzania iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na  Mchezaji bora alikuwa Diana Lucas wa Tanzania.


Kwenye mchezo dhidi ya Eswatin ambapo Tanzanite iliinyoosha kwa mabao 8-0 na mchezaji bora alikuwa Diana Lucas wa Tanzania


 Tanzanite dhidi ya Zambia ambapo tulipoteza kwa kunyooshwa kwa mabao 2-1 n mchezo wa mwisho wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Afrika Kusini Tanzanite ilishinda mabao 2-0 na mchezaji bora kuwa  Enekia Kasonga wa Tanzania.

DUH KUMBE LUKAKU ALIKUWA UNITED MAWAZO YAKE JUMLA YAPO INTER MILAN TOWNSHIP ROLLERS WATUA NA MAJI YAO DAR KUCHEZA NA YANGA TAIFA – VIDEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply