Home Uncategorized MABINGWA SIMBA WAANZA KUWATISHA UD do SONGO, KUPIGA MAZOEZI YA MWISHO LEO

MABINGWA SIMBA WAANZA KUWATISHA UD do SONGO, KUPIGA MAZOEZI YA MWISHO LEO


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kwa sasa wameshatia timu nchini Msumbuji kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kesho dhidi ya UD do Songo utakaochezwa kesho.

Simba imekwea pipa leo asubuhi kutoka Bongo kwa dege binafsi ili kukwepa usumbufu na wanatarajia kurejea kesho baada ya kumaliza mchezo huo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

Simba leo itafanya mazoezi jioni kwa ajili ya kujiweka sawa kuwavaa mabingwa hao wa Msumbiji.

SOMA NA HII  RATIBA LIGI KUU BARA LEO IPO HIVI