Uncategorized

NYOTA SIMBA KUIBUKIA NAMUNGO FC, DILI YA AFRIKA KUSINI YABUMA

admin August 11, 2019 2:49 pm


ADAM Salamba mchezaji wa Simba dili lake la kujiunga na timu ya Polokwane FC ya Afrika Kusini limebuma na sasa anarejea Bongo kujiunga na kikosi cha Namungo FC.

Salamba ambaye alisajiliwa na Simba msimu wa 2018/19 akitokea Lipuli FC ameshindwa kwenda na kasi ya Simba na ametolewa kwa mkopo.

Awali Polokwane FC walikuwa wanahitaji huduma yake, habari zinaeleza kuwa hawajafika mwafaka na uongozi ambao umeamua kumpeleka Namungo

Salamba amesema kuwa msimu ujao ataitumikia timu hiyo yenye ngome yake Lindi.

HALI YA MLINDA MLANGO NAMBA MOJA WA LIVERPOOL BADO KIZUNGUMKUTI ROLLERS: YANGA SIO WA MCHEZOMCHEZO, TUTAPAMBANA NAO KIBISHI NYUMBANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply