Uncategorized

TANZANITE KUMALIZANA NA ZAMBIA LEO COASAFA

admin August 11, 2019 1:39 am


TIMU ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ leo itakuwa kazini kumenyana na timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia.

Tanzanite imealikwa kwenye michuano hii ya COSAFA inayofanyika nchini Afrika Kusini.

Kwenye hatua ya makundi Tanzanite ilipoteza mchezo mmoja pekee dhidi ya Zambia ambao wanacheza nao leo.

Dakika 90 kwenye mchezo wa kwanza, Zambia ilishinda mabao 2-1 na kuibuka wababe mbele ya Tanzanite inayonolewa na Kocha Mkuu Bakari Shime.

Mchezo wa kwanza Tanzanite iliwanyoosha Botswana mabao 2-0 kabla ya kujipigia Eswatini mabao 8-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Shime amesema kuwa fainali siku zote haina mwenyewe hivyo watakazana kupata matokeo,.

“Fainali sio kitu chepesi, tuna kazi ngumu na kubwa, tunawaheshimu wapinzani wetu hivyo tunaingia kwa tahadhari kwa kuwa walitufunga mchezo wa kwanza,” amesema.

JESHI LA KMC KIMATAIFA LEO HILI HAPA DHIDI YA AS KIGALI MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA JUMAPILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply