Uncategorized

NAIBU WAZIRI WA HABARI, SANAA, MICHEZO NA UTAMADUNI AKABIDHI KOMBE KWA MABINGWA WA NDONDO CUP UV TEMEKE

admin August 12, 2019 6:19 am


NAIBU Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Juliana Shonza amewakabidhi kombe la Ndondo Cup timu ya UV Temeke, yenye maskani yake Temeke jana baada ya kuwanyoosha wapinzani wao Uruguay.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Bandari ulikuwa ni wa kukata na shoka kwa timu zote kuhaha kutafuta matokeo.

Licha ya Uruguay kupachika bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Chinu Mbaya halikudumu kwani UV Temeke waliweka mzani sawa kupitia kwa Hamis Ngoengo.

 
UV Temeke imetwaa ubingwa huo kwa ushindi wa penalti 5-3.

KOCHA TANZANITE AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO SIMBA WAIVUTIA PUMZI UD SONGO, MAKALI YAO YOTE KWA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply