Uncategorized

SIMBA WAIVUTIA PUMZI UD SONGO, MAKALI YAO YOTE KWA AZAM FC

admin August 12, 2019 6:19 am


PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hesabu kubwa ni mchezo wake wa ngao ya jamii dhidi ya Azam FC utakaopigwa Jumamosi uwanja wa Samora, Iringa.

Aussems amesema mpango wa mechi ya kimataifa dhidi ya UD do Songo ameuweka kando kwa muda. 


“Hesabu kubwa ni kuona tunapata matokeo kwenye mchezo wetu dhidi ya Azam ambao utaanza kabla ya marudiano na UD do Songo.

 “Nikimaliza kucheza na Azam nitakuwa na muda wa kuifikiria UD do Songo na nina amini utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani,” amesema.

Mchezo wa kwanza wa kimataifa hatua ya awali Simba ililazimisha sare dhidi ya UD Songo ya Msumbiji hivyo wana kazi kupata matokeo mechi ya marudiano ili kusonga mbele inayotarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25.

NAIBU WAZIRI WA HABARI, SANAA, MICHEZO NA UTAMADUNI AKABIDHI KOMBE KWA MABINGWA WA NDONDO CUP UV TEMEKE YANGA YAPANIA KUPINDUA MEZA KIBABE BOTSWANA, SARE YAWAUMIZA KINOMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply