Uncategorized

YANGA YAPANIA KUPINDUA MEZA KIBABE BOTSWANA, SARE YAWAUMIZA KINOMA

admin August 12, 2019 6:34 am


MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kazi kubwa aliyonayo sasa ni kusuka mpango makini utakaowapa matokeo ugenini.

Karata ya kwanza kwenye michuano ya kimataifa Yanga imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Township Rollers Uwanja wa Taifa.


 “Wachezaji wangu wamefanya makosa ambayo yanarekebishika, sikupanga kupata sare nyumbani hasa ukizingatia michuano hii ya kimataifa kila mmoja anajivunia nyumbani.

 “Tuna mechi moja mkononi hiyo ndiyo tiketi yetu muhimu, wao wamepata bao nyumbani nasi tunakwenda kufanya kweli, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Rollers ilipachika bao dakika ya saba kupitia Kwa Phenyo Serameng kabla ya Patrick Sibomana kuweka usawa dakika ya 86 kupitia mkwaju wa penalti uliomshinda mlinda mlango Wagare Dikago.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 23-25, Botswana.

SIMBA WAIVUTIA PUMZI UD SONGO, MAKALI YAO YOTE KWA AZAM FC KMC LEO WACHEZAJI NI MWENDO WA BATA, KMKM MLIMA MZITO, MALINDI PIA MOTO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply