Uncategorized

KMC LEO WACHEZAJI NI MWENDO WA BATA, KMKM MLIMA MZITO, MALINDI PIA MOTO

admin August 12, 2019 6:54 am

JACKSON Mayanya, Kocha Mkuu wa KMC amewapa mapumziko ya siku moja wachezaji wake kabla ya kuanza mazoezi kesho kuiwinda AS Kigali hivyo kazi ni kwao kula Bata

KMC ina kibarua cha kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya AS Kigali ya Rwanda.

Sare ya bila kufungana bao italeta matumaini iwapo watashinda mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa kati ya Agosti 23-24.

Wawakilishi wa Zanzibar, KMKM wana kazi kubwa ya kutafuta matokeo mbele ya 1st de Agosto ya Angola baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 Uwanja wa Amaan kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na itarudiana nao Agosti 24.

Malindi wao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho ina kazi ya kutafuta ushindi nyumbani baada ya kulazimisha Sare ya bila kufungana ugenini dhidi ya Mogadishu City ya Somalia.
YANGA YAPANIA KUPINDUA MEZA KIBABE BOTSWANA, SARE YAWAUMIZA KINOMA KUWAONA WA KIMATAIFA SIMBA NA AZAM FC TAIFA BUKU TANO TU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply