Uncategorized

KISA ITC FAROUK NA WENZAKE WAWILI KUIKOSA TOWNSHIP ROLLERS WIKI IJAYO, PIGO YANGA

admin August 18, 2019 9:01 am


Inaelezwa kuwa kipa namba moja wa Yanga aliyesajiliwa hivi karibuni Farouk Shikalo ataukosa mchezo wa marejeano baina ya timu yake na Township Rollers katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbali na Shikalo, beki Mustapha Seleman pamoja na mshambuliaji David Molinga ‘Falcao’ naye anaweza kuwa si sehemu ya mchezo huo.

Sababu za kukosekana kwa wachezaji hawa ni kukosa leseni kutoka CAF na kuchelewa kutumwa kwa ITC zao.

Kwa sasa uongozi wa Yanga upo katika harakati za kupambana kusaka leseni za wachezaji hao ili kuongeza morali na nguvu ya timu kuelekea mechi hiyo kubwa.

Yanga inaenda kucheza na Rollers August 23 ikiwa na kumbukumbu ya kwenda sare ya 1-1 kwenye mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MO AZUIA PRESS YA HAJI MANARA SIMBA RATIBA YA MICHUANO YA CECAFA KWA TIMU YA TAIFA CHINI YA MIAKA 15

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply