Uncategorized

AGOSTI 30 MZIZIMA BOXING FAMILY GROUP KUKIWASHA, MASHABIKI WAITWA KUPATA UHONDO

admin August 19, 2019 11:35 pm


MWENYEKITI wa kundi la Mzizima Boxing Family Group (MBFG), Dr.Abdallah Mandai amewataka mashabiki wa mchezo wa boxing kujitokeza kwa wingi Agosti 30 ukumbi wa CCM Ilala Kata kushuhudia vipaji kwa vijana watakaopanda ulingoni.

Mashindano hayo ndiyo ambayo yaliweza kuwatengeneza mabondia maarufu Bongo kitaifa na kimataia kama Rashid Matumla, Francis Cheka na wengine wengi.

 Akizungumza na Saleh Jembe, Mandai amesema kuwa lengo kubwa la kundi hilo ni kuinua vipaji kwa vijana wenye uwezo wa kupambana ulingoni.

“Tunajua kwamba kuna vijana wenye uwezo wa kupambana na hawapati nafasi hivyo ni fursa yao sasa kuonyesha namna gani wanaweza kupata nafasi.

“Agosti 30 ni siku nzuri kwa mashabiki wa boxing kujitokeza kuona namna ushindani wa vijana ulivyo, kuna vijana zaidi ya 100 ambao watapanda kwenye ulingo kwa utaratibu maalumu hivyo tunawaomba mashabiki wajitokeze,” amesema.

ZAHERA: ZIARA YA ARUSHA NA MOSHI IMETUPOTEZEA MUDA WETU, HAINA MAANA – VIDEO AZAM FC YASAHAU MAUMIVU YA KUPOTEZA NGAO YA JAMII, SASA NI MWENDO WA KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply