Uncategorized

SIMBA YAWATAKA MASHABIKI KUZIUNGA MKONO YANGA, KMC NA AZAM FC KIMATAIFA

admin August 21, 2019 6:49 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa thamani ya mashabiki kwa klabu yao ni kubwa kuliko chochote kwani wao wanabeba siri ya mafanikio.


Jumapili ya wiki hii, Simba itakuwa Uwanja wa Taifa ikimenyana na UD Songo mchezo wa marudio wa kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ue wa awali nchini Msumbiji kutoka sare ya bila kufungana.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:”Kwetu mashabiki sio mchezaji wa 12, ni mchezaji wa kila nafasi uwanjani.Tunashinda lakini mashabiki wanachangia sana”.

Simba pia imewataka mashabiki kuziunga mkono timu nyingine ambazo ni KMC, Azam FC ambazo zitakuwa nyumbani pamoja na Yanga ambao wao watakuwa ugenini.
MENEJA WA MACHESTER UNITED AMKINGIA KIFUA POGBA CLUB 361 INAKULETEA MAPAMBANO YA UBINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply