Uncategorized

DEMBELE AIHARIBU BARCELONA

admin August 22, 2019 9:03 pm


WINGA wa Barcelona, Ousmane Dembele ameanza vitimbi baada ya majuzi kudaiwa kwenda zake nchini Senegal kwa shughuli ya kifamilia. Dembele alidaiwa kuwa aliwaficha madaktari maumivu ya paja aliyokuwa nayo na badala yake akaenda zake Senegal.

Winga huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa inasemekana alilala kwenye uwanja wa ndege wa
Bilbao ili kusubiri ndege ya kwenda Dakar, Senegal baada ya mechi na Athletic Bilbao.

Baada ya mchezo huo na Bilbao inasemekana daktari wa Barcelona, Xavi Yanguas alimuuliza Dembele kama yupo vizuri. Dembele alidai yupo sawa ingawa Yanguas alimtafuta siku inayofuata kwa ajili ya vipimo zaidi lakini staa huyo hakuonekana.

Badala yake aliripoti mazoezi ya wiki hii, ambapo inadaiwa alipofanya mazoezi kidogo akawa analalamika maumivu na alivyopimwa paja lake ikaonekana inabidi apumzike kwa wiki tano.

POFBA APIGWA STOP MAN UNITED TFF YA BOTSWANA YAIRAHISHIA KAZI YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply