Uncategorized

YANGA YATOA DOZI KWA WABOSTWANA, AZAM NAYO MWENDO MDUNDO, YATOA KICHAPO CHA MAANA

admin August 24, 2019 3:43 pm

Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Taifa wa Bostwana kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Township Rollers katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Yanga imepata ushindi mnamo dakika ya 42 kupitia kwa Juma Balinya aliyefunga kwa mkwaju wa faulo.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam, Yanga iliweza kwenda sare ya bao 1-1.

Kipa wa Yanga Metacha Mnata aliweza kudaka penati ya Rollers kipindi cha pili na kuweza kuipunguzia kazi ya kuanza kusaka bao jingine.

Ukiachana na Yanga, Azam FC pia ilikuwa na mchezo leo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo imefanikiwa kuichakaza vibaya Fasil Kenema kwa mabao 3-1 ambapo katika mechi ya kwanza walifungwa 1-0.
LIIVE!! TOWNSHIP ROLLERS 0-0 YANGA, LIGI YA MABINGWA AFRIKA MANARA AVUNJA UKIMYA, AFUNGUKA KUHUSIANA NA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply