Uncategorized

KOCHA SIMBA AJA KIVINGINE KABISA, ATAJA MALENGO TOFAUTI

admin August 26, 2019 4:32 pm


Na George Mganga

Baada ya kuondolewa jana katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amekuja kivingine.

Aussems ameamua kuja na malengo ambayo kwa sasa ni kuhakikisha wanafanya vema katika mashindano yote yanayiowakabili ikiwemo taji la FA.

Kauli hiyo imekuja kutokana na Simba kuondolewa kwenye mashindano hayo makubwa na UD Songo kwa sare ya bao 1-1, mechi ikipigwa Uwanja wa Taifa.

“Malengo yetu kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye mashindano yote kuanzia Ligi Kuu, kombe la FA na mingine ambayo tutashiriki, ” amesema Aussems.

Simba imeondoshwa mashindano kutokana na faida ya bao la ugenini ambapo katika mechi ya kwanza huko Msumbiji ililazimishwa suluhu ya 0-0.

REKODI YA DAVID SILVA NDANI YA MANCHESTER CITY TAMU SANA ZAHERA ATOBOA SIRI YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply