Home Uncategorized YANGA YACHOMOLEWA BETRI MOJA BILA KWA YAI RUVU SHOOTING WAKIFUTA UTEJA DAR

YANGA YACHOMOLEWA BETRI MOJA BILA KWA YAI RUVU SHOOTING WAKIFUTA UTEJA DAR


Na George Mganga

Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Taifa kwa Yanga kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwa timu hizo mbili.

Bao pekee na Ruvu Shooting limewekwa kimiani na Sadat Mohammed akimvisha kanzu kipa Farouk Shikalo mnamo dakika ya 20 kipindi cha kwanza.

Bao hilo limeweza kudumu kwa dakika zote 90 mpaka Mwamuzi Martin Saanya alipohitimisha mchezo wa kupuliza kipyenga cha mwisho, ubao ukisomeka 1-0.

Katika mechi hiyo, Kocha Mwinyi Zahera aliwatoa wachezaji Sadney Urikhob na kumwingiza Maybin Kalengo, Juma Balinya akimtoa pia na nafasi yake akichukua Balama Mapinduzi lakini mabadiliko hayakuleta mafanikio.

Ruvu imeweka rekodi kwa mara ya kwanza kufuta uteja kwa Yanga tena ikiibuka mshindi ikiwa ugenini.

Kama mdau wa michezo, unaweza kutuambia Yanga waliteleza wapi? Ndondosha maoni yako hapo chini.


SOMA NA HII  BAADA YA BIRIANI LA SIMBA KULIWA,NENO LAO HILI HAPA