Home Uncategorized ARSENAL WASHINDA KIBABE MBELE YA BURNLEY, YAJIPIGIA VIDUDE VIWILI

ARSENAL WASHINDA KIBABE MBELE YA BURNLEY, YAJIPIGIA VIDUDE VIWILI

[the_ad id="25893"]


MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Pierre Aubameyang amesema kuwa anajiskia furaha kwa timu yake kushinda leo mbele ya Burnley mchezo wa pili wa Ligi Kuu England baada ya kuanza kushinda mbele ya Newcastle United.

Arsenal leo imeshinda mabao 2-1 ambapo bao la ushindi la Arsenal limepachikwa na Aubameyang dakika ya 64 na kuipa pointi tatu muhimu tmu yake na lili la kwanza lilifungwa na Laccazette dakika ya 13 na lile la kufutia machozi likifungwa na Ashley Barnes dakika ya 43.

“Najiskia faraja kupata ushindi kwa timu yangu kwani haikuwa kazi nyepesi na tumepambana kupata matokeo kwenye mchezo wa leo,” amesema Aubameyang.

Hili linakuwa ni bao lake la pili msimu huu ndani ya Ligi Kuu England mshambuliaji Auba.

SOMA NA HII  KUHUSU KUTUA SIMBA..MENEJA WA MWANYETO AMEFUNGUKA HAYA..!!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here