Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa halitakuwa na huruma kwa klabu yoyote itakayotaka kubadili rangi ya nembo ya wadhamini wao kwa msimu huu wa 2019/20 katika Ligi Kuu Bara.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya Rais wa TFF kupitia Rais wake, Wallace Karia, kuingia mkataba mwingine wa udhamini na benki ya KCB.
Karia amesema hivyo akieleza wadhamini wanapaswa kuheshimiwa hivyo haitaruhusiwa timu yoyote ile kuvaa jezi ambazo hazina nembo yenye rangi rasmi ya mdhamini.
Aidha, Karia amesema kuwa kwa baadhi ya makocha wanaoingia uwanjani na jezi zenye nembo ya makampuni mengine tofauti na za wadhamini wanaotambulika na TFF lazima wawachukulie hatua.
Kauli hii inakuwa inazidi kuleta wakati mgumu kwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye amekuwa akivaa tisheti zenye nembo ya POLO sambamba na klabu yake ambayo inaelezwa imegomea kuvaa jezi zenye nembo nyekudu kutoka Vodacom.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.