HASSAN Mwakinyo, bondia wa ngumi za kulipwa Bongo ambaye ni balozi wa kampuni ya kubashiri ya SportPesa ameiomba Serikali kuongeza nguvu ya uwekezaji kwa upande wa mchezo wa ngumi kama ilivyo upande wa soka.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mwakinyo amesema kuwa mabondia wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi na nguvu kuitangaza Tanzania mwisho wa siku thamani yao inakuwa ya kawaida pale wanapoishiwa na nguvu.
“Kazi yetu ni kubwa na ngumu, Serkali inatupa sapoti ila bado kuna uhitaji mkubwa kwetu ukizingatia kila iitwapo leo mabondia wengi wanaibuka na wanafanya vizuri itape ndeza endapo sapoti itaongezeka kwetu pia.
“Tunaona mabonasi ambayo wanapewa wachezaji wa mpira, huwa inafika pesa nyingi na thamani yao inakuwa kubwa itapendeza nasi pia tukitazamwa kwa jicho la pekee ili kuongeza moyo wa kufanya zaidi.
“Jambo pekee ninalojivunia ni kwamba Serikali yetu ni sikivu ndio maana ni miongoni mwa wale walioitwa na Rais Ikulu kwa sasa napambana ili kufanya makubwa zaidi,” amesema.
Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni Octoba 26 uwanja wa Taifa ambapo mabondia kutoka nchini Argentina, Marekani, Kenya wapo tayari kupambana naye.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.