Uncategorized

SIRI YA NEYMAR YAFICHUKA REAL

admin September 5, 2019 10:13 am


Sababu kuu tatu ndizo zinaelezwa kuwa zilisababisha Real Madrid kuachana na mpango wa kumsajili staa wa Paris St. Germain, Neymar. Pamoja na baba wa Neymar kuwabembeleza sana Real Madrid lakini klabu hiyo haikushawishika kumvuta staa huyo.

Habari za kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa klabu hiyo ilifuta mpango wa kumsajili staa huyo kutokana na matakwa makubwa ya fedha ya PSG.

PSG kwa kiasi kikubwa ilikuwa inataka kurudisha gharama zao za pauni milioni 199 walizotumia kumsajili Neymar kutoka Barcelona mwaka 2017.

Inaelezwa kuwa sababu nyingine ni kutokana na Neymar mwenyewe kuwa na dhamira ya kurudi Barcelona.

Sababu ya tatu inadaiwa kuwa Real Madrid walikuwa na mashaka na kama staa huyo kama atakuwa fiti kutokana na kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwa sababu ya majeraha.

Habari za ndani za PSG zinasema kuwa uongozi wa klabu hiyo walikuwa hawataki kusikia habari ya Barcelona kwa kukumbuka walivyowasumbua wao kumpata Neymar.

JUMA ABDUL APATWA NA PIGO KUBWA, AFIWA NA MAMA YAKE WALIOOA FC VS WASIOOA KESHO HAPATOSHI UWANJA WA CHUO CHA USTAWI DAR

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply