Uncategorized

YANGA YAZIPIGIA HESABU NDEFU PESA ZA CAF

admin September 5, 2019 11:18 am


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unajipanga kufanya vema kwenye michuano ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ili kufikia hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kuvuna mkwanja mrefu.

Yanga itamenyana na Zesco Septemba 14 uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa hatua ya kwanza kabla ya kutinga hatua ya makundi.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa hesabu kubwa ni kuona kikosi kinafanya makubwa ili kupata fedha kwa ajili ya matumizi ya klabu.

“Timu ikishinda na kupenya hatua  ya makundi kuna fedha ambazo timu itapata tena ni nyigi hapo itakuwa rahisi kwetu kuziweka kwenye matumizi yetu ya timu.

“Kila kitu kinawezekana ukizingatia kwamba tuna kikosi kipana na kilicho imara, mashabiki watupe sapoti ili tufikie malengo yetu,” amesema. 

WALIOOA FC VS WASIOOA KESHO HAPATOSHI UWANJA WA CHUO CHA USTAWI DAR AZAM FC YAPANIA KUFANYA MAKUBWA MBELE YA WAZIMBABWE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply