Home Uncategorized NYOTA STARS : ITAKUWA BAHATI KWA BURUNDI KUPONA TAIFA

NYOTA STARS : ITAKUWA BAHATI KWA BURUNDI KUPONA TAIFASIMON Msuva, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania amesema kuwa itakuwa ngumu kwa Burundi kupenya Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa kwanza wa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia uliofanyika nchini Burundi timu zote zilitoshana nguvu Kwa kufungana bao 1-1.

Msuva amesema matokeo hayo yanaipa nafasi timu ya Taifa kupata matokeo chanya mchezo wa marudio. 


“Matokeo ya Sare ambayo tumeyapata sio mabaya sana tofauti na kama tungekuwa tumepoteza kabisa sasa ni nafasi yetu kushinda mchezo wa marudio na hatupaswi kuwadharau wapinzani,” amesema.

Stars itamenyana na Burundi Septemba nane uwanja wa Taifa na kinachotakiwa ni ushindi ili timu isonge mbele hatua ya makundi.
SOMA NA HII  NAFASI YA CIOABA YAGOMBEWA KAMA NJUGU AZAM FC

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here