Uncategorized

KIMENUKA!! MCHEZAJI YANGA AAMUA KUKIWASHA, AMKATAA KOCHA MPYA

admin January 15, 2020 9:57 pm

Baada ya kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa jana kunako Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakali Malima, amesema timu haikustahili kubadilisha kocha.

Malima ameeleza kuwa Yanga ilipaswa kuendelea kumwamini na kumtumia Mkwasa sababu tayari alikuwa ameshaanza kuwaweka sawa wachezaji kitimu.

Mchezaji huyo amefunguka akieleza kuwa Mkwasa alikuwa ameshaanza kuwapa somo wachezaji baada ya aliyekuwa kocha Mwinyi Zahera kuwaacha na walianza kuja vizuri lakini ameshangazwa na Yanga kumtoa Mkwasa.

“Unajua Yanga mimi nawashangaa sana kuleta kocha mwingine.

“Mkwasa tayari alikuwa ameshaanza kuwapa somo vijana na walianza kumwelewa, kwanini tena waachane naye na walete kocha mwingine.

“Sijaafiki, kuleta kocha mwingine kunazidi kuirudisha timu nyuma na ni maamuzi ambayo mimi sijayapenda.”
MAN UNITED YAIPIGA CHINI BARCELONA SERIKALI YAHOJI KUHUSIANA NA BILIONI NNE ZA MO DEWJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply