Mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta amefikia makubaliano na klabu ya Aston Villa ya England.
Samatta anatarajia kujiunga na Aston Villa ambayo inashiriki Ligi Kuu England.
Aston Villa imekubali kulipa dau la pauni milioni 10 ili kumpata Samatta ambaye msimu uliopita alikuwa kinara wa ufungaji mabao katika kikosi hicho cha Ubelgiji.