Uncategorized

BAADA YA NAFASI KUCHUKUA MZUNGU, MKWASA AFUNGUKA JUU YA HATMA YAKE NA YANGA

admin January 16, 2020 9:32 pm

Aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kuwa hajui hatima yake ndani ya klabu hiyo mara baada ya ujio wa kocha mpya Mbelgiji, Luc Eymael.

Yanga imemleta Eymael kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera ambapo Mkwasa alikuwa akikaimu kwa muda tangu kutimuliwa kwa Zahera mwishoni mwa mwaka jana.

Mkwasa amesema kuwa, kwa sasa bado hajui hatima yake ndani ya kikosi hicho baada ya kocha mpya licha ya kuendelea kuwepo kikosini, huku akisema hafahamu kama atabaki au la.

“Tumefurahi ujio wa kocha mpya ndani ya Yanga na tutatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha anafanya kazi vizuri kwa kumuelekeza utaratibu wote wa timu.

“Kwa upande wangu bado sijajua hatma yangu viongozi ndiyo wanaojua na ndiyo wenye majibu kuhusu uwepo wangu ndani ya timu, kwa sasa bado naendelea kukinoa kikosi hadi kocha mpya atakapotambulishwa rasmi kwani kwa sasa bado hajakabidhiwa kikosi,” alisema Mkwasa
SOMO LA KATUMBI KWA MO DEWJI JUU YA UWEKEZAJI YANGA WATOKWA NA MACHOZI, INATIA HURUMA – VIDEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply