Uncategorized

MEDDIE KAGERE AZUA GUMZO SIMBA, REKODI ZATAJWA

admin January 26, 2020 9:13 pm


GUU la kulia na staili za mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, zimezua gumzo. Guu hilo limeweka rekodi kwa kuwaliza makipa  sita wa Bongo tofauti na lile la kushoto lililomuotea kipa mmoja tu.

Lakini rekodi za msimu huu zinaonyesha bichwa lake pia ni balaa, limewalaza macho makipa watatu. Kwenye mabao yake 11, guu lake la kulia limekutana na makipa hawa; Farouk Shikalo wa Yanga (Simba 2-2 Yanga), Said Kipao wa Kagera Sugar (Kagera Sugar 0-3 Simba), Shaban Hassan wa Mtibwa Sugar(Simba 2-1 Mtibwa Sugar).

Richard Peter wa Mbeya City(Simba 4-0 Mbeya City)  na Agathony Mkwanda wa Lipuli (Simba 4-0 Lipuli) waliokoteshwa mara mojamoja kila mmoja na Abdulrahman Mohamed wa JKT Tanzania aliokoteshwa nyavuni mara mbili wakati Simba ikishinda mabao 3-1. Kwa guu la kushoto ni Daniel Johannes wa Biashara United alikutana na balaa wakati Simba ikishinda mabao 2-0.

Ametupia jumla ya mabao matatu kwa kichwa ambapo aliwaokotesha nyavuni Mwadini Ally wa Azam FC,(Simba 1-0 Azam), Said Kipao wa Kagera Sugar(Kagera Sugar 0-3 Simba) na John Mwenda wa Alliance (Alliance 1-4 Simba), hawa wote aliwatungua bao mojamoja.
MORRISON APEWA MAJUKUMU YANGA KISA SIMBA, GSM AFANYA KUFURU NYINGINE YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply