Uncategorized

SIMBA YATAJA INACHOKITAKA KWA NAMUNGO LEO

admin January 29, 2020 1:52 pm


JONAS Mkude, kiungo wa Simba ambaye amedumu kwa muda mrefu amesema kuwa leo ndani ya Uwanja wa Taifa wana kazi moja tu ya kutafuta pointi tatu muhimu.

Simba itamenyana na Namungo ya Lindi Uwanja wa Taifa, mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kukutana kwa timu hizi mbili ndani ya ardhi ya Bongo.

Mkude amesema: “Tunatambua kwamba ligi sio kitu chepesi na kila timu ni bora kikubwa ambacho tunafikiria ni kuona namna gani tunapata pointi tatu ambazo zitatupa mwanga wa kule ambako tunakwenda,” amesema.

Kwenye mechi mbili za mwisho wakati Simba ikikusanya pointi sita za kanda ya ziwa, Uwanja wa CCM Kirumba, Mkude alifunga jumla ya mabao mawili na alitoa pasi moja ya bao.

STARTIMES IPO KWA AJILI YA JAMII, MATUKIO YAKE YA 2019 HAYA HAPA, TUZO PIA ZIPO JESHI LA NAMUNGO LEO DHIDI YA SIMBA, PAU BUKABA AANZIA BENCHI, BAROLA NDANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply