Uncategorized

SIMBA YAIPIGIA HESABU JKT TANZANIA KESHO, TAIFA

admin February 6, 2020 12:09 pm

UONGOZI wa Simba umesema kuwa timu itaendelea kupambana kwenye mechi zake zote za Ligi Kuu Bara ili kufikia malengo waliyojiwekea ya kutetea ubingwa msimu huu.

Simba kesho itashuka Uwanja wa Taifa kumenyana na JKT Tanzania ikiwa ni mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili kwa msimu wa 2019/20.

Akizungumza na Saleh Jembe, Patrick Rweyemamu, Meneja wa Simba amesema kuwa wachezaji wapo salama na wanaendelea kujipanga kwa ajili ya mechi zao.

“Wachezaji wapo vizuri na masuala yote ya kiufundi yapo chini ya Kocha Mkuu (Sven Vanderbroeck) tuna matumaini ya kuendelea kuyafuata malengo ambayo tumejiwekea, mashabiki watupe sapoti,”.

Mchezo wa kwanza Simba ilipokutana na JKT Tanzania ilishinda kwa mabao 3-1, Uwanja wa Uhuru, kesho itakutana nao tena Uwanja wa Taifa ikiwa kileleni na pointi 50 huku JKT Tanzania ikiwa nafasi ya 8 na pointi 27.

NAMUNGO: MOTO WA LIGI KUU BARA SI MCHEZO KOCHA MANCHESTER UNITED: FERNANDES BADO HAJAFIKIA KUWA RONALDO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply