Uncategorized

AZAM FC KUHAMISHIA HASIRA ZA PRISONS KWA KMC

admin February 7, 2020 6:14 am

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utapambana kupata pointi tatu muhimu mbele ya KMC watakapokutana kesho, Februari,8, Uwanja wa Uhuru.

Azam FC itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kubanwa mbavu na Tanzania Prisons kwa kufungana bao 1-1 mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Uhuru huku KMC ikiitandika bao 1-0 Mbeya City, Samora.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC Jaffary Maganga amesema kuwa wanaitambua vema KMC ni timu imara wataingia kwa tahadhari kubwa.

“Ni timu nzuri KMC ila tutawafuata kwa tahadhari kubwa ili kuona namna gani tutashinda mchezo wetu na kuchukua pointi tatu muhimu,” amesema.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru wakati huo KMC ikiwa chini ya Jackson Mayanja na Azam chini ya Ettiene Ndayiragije, Azam ilisepa na pointi tatu muhimu.

JKT TANZANIA; MECHI YETU DHIDI YA SIMBA NI NGUMU, ILA TUNAZITAKA POINTI TATU RUVU SHOOTING YAIPIGA MKWARA MWINGINE YANGA, YATAKA MABAO MENGI KINOMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply