Uncategorized

INTER MILAN WASEPA NA KIJIJI KIZIMA CHA ENGLAND

admin February 13, 2020 3:07 pm


INTER Milan inayoshiriki Serie A, Ligi Kuu ya nchini Italia inaonekana kuchukua nyota wengi kutoka Premier League.

Ndani ya msimu mmoja imewapa shavu nyota watano ambao wanakipiga ndani ya klabu hiyo kwa sasa.

Christian Eriksen raia wa Denmark aliyekuwa kiungo ndani ya Spurs ametua pia Inter Milan kwenye usajili wa dirisha dogo.

Pia Victor Moses aliyekuwa anakipiga Chelsea naye amevutwa ndani ya kikosi hicho kwa mkopo, aliyekuwa nahodha wa Manchester United, Ashley Young naye pia yumo ndani.


Alexis Sanchez alitua kwa mkopo na Romelu Lukaku alisajiliwa jumla ndani ya kikosi hicho.

Bosi pia wa timu hiyo Antonio Conte aliinoa Chelsea kuanzia 2016/2018, Paolo Vanoli yupo kwenye benchi la ufundi alikuwa pia Chelsea.


Inter Milan ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 54 sawa na wapinzani wao Juventus wakipishana kwenye idadi ya mabao ya kufunga ambapo Juve wana mabao 44 huku Inter Milan wakiwa na mabao 48.

KOCHA SIMBA APEWA ONYO KALI NA BODI YA LIGI, POLISI TANZANIA WAVURUMISHWA FAINI HAWA HAPA WATAJWA KUWA KISIKI CHA MPINGO KWA LIVERPOOL EPL

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply