Uncategorized

SINGIDA UNITED INATAFUTA DAWA YA TATIZO LAO

admin February 13, 2020 4:37 am
KIKOSI cha Singida United kilicho chini ya Ramadhan Nswanzurimo juzi kilibanwa mbavu na Namungo FC kwa kufungwa bao 1-0 mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Liti ambao zamani ulikuwa unaitwa Namfua.
Singida United ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 imeshinda mechi mbili, imepoteza mechi 14 na kulazimisha sare tano na kibindoni ina pointi 11.
Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa kikosi hicho kinapata tabu msimu huu jambo ambalo wanalifanyia kazi kwa ukaribu.
“Mashabiki wanakasrika kuona timu inapoteza hata viongozi pia hatufarihishwi kuona kikosi kinapata tabu kupata matokeo, kwa sasa tunatafuta dawa ya tatizo na mambo yatakuwa mazuri,” amesema Katemana.
Kwenye dirisha dogo la usajili, Singida United iliongeza wakongwe wengi ikiwa ni pamoja na Athuman Idd ambaye ametoa pasi moja ya bao kwenye mchezo dhidi ya Yanga ambao Singida United walipoteza kwa kufungwa mabao 3-1.
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA ALHAMISI HIVI NDIVYO ABAROLA WA AZAM ALIVYOWANYIMA POINTI WAPINZANI WAKE KWA KUOKOA PENALTI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply