Uncategorized

WAANDISHI WAMPONZA AGGREY, APIGWA FAINI NA BODI YA LIGI

admin February 13, 2020 2:37 pm




Ile tabia ya baadhi ya wachezaji na makocha kuwadharau waandishi wa habari kuhusiana na suala la mahojiano imemtokea puani nahodha wa Azam FC, Aggrey Morris.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari  10, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;

Mechi namba 189:Azam Fc 1 vs Tanzania Prisons Fc 1

Morris amepigwa faini ya kiasi cha Tsh 200,000/=(Laki Mbili) kwa kosa la kugoma kuongea na  waandishi wa habari  mara baada ya mchezo kumalizika katika mechi iliyochezwa Februari 05,2020 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Adhabu hii imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

LICHA YA KUCHIMBISHWA SPURS, MUARGENTINA POCHENTINO ANA REKODI TAMU KWELI MWAMUZI WA KONA YA MAAJABU YA YANGA AFUNGIWA NA BODI YA LIGI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply